8 Julai 2015 - 18:40
Watu 44 wauwawa katika mripuko uliotekea nchini Nigeria

Kutokana na miripuko iliotokea na milio ya risasi katika mgahawa mmoja na msikiti katika wilaya ya Jusi nchini Nigeria nakusababisha vifo vya watu 44 na wengine 47 kujeruhiwa katika tukio hilo

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: miripuko ya mabomu hayo mawili yametokea katika wilaya ya Jusi nchini Nigeria imesababisha mauaji ya watu 44 katika tukio hilo, huku ripoti zinaonyesha kuwa bomu la kwanza liliripuka nje ya mgahawa huo na bomu la pili liliripuka karibu na msikiti huku risasi zikipigwa katika msikiti huo.
Kwamujibu wa ripoti za serikali zinaeleza kuwa watu 23 wamefariki baada ya kuripuka bomu la kwanza karibu na mgahawa katika wilaya hiyo, ama watu wengine 21 wamefariki baada ya kuripuka bomu la pili mkabala na msikiti huo huku risasi ziliokuwa zikipigwa katika msikiti huo.
Baadhi ya ripoti zinaashiria kuwa lengo la kutega mabomu hayo ni kumtafuta mwanazuoni mmoja ambaye hapo mwanzo alitishiwa maisha yake na kikundi cha kigaidi cha Book Haram.
Pia siku iliopita kuliliripuliwa bomu katika kanisa moja tukio ambalo limesababisha kuwawa watu 6 nchini humo, mpaka sasa hakuna kikundi chochote kilichotangaza kuhusika na matukio hayo ya kigaidi, ama hali ya wilaya Jusi kabla ya matukio hayo inaonyesha kuwa mara kadhaa magaidi wa Book Haram waliishambulia wilaya hiyo na kufanya mashambulio katika sehemu hiyo.
Kushadidi miripuko nchini Nigeria kumesababisha khofu kubwa kwa wananchi wa nchi hiyo kiasi kwamba faida ya kuwepo jeshi la kukabiliana na magaidi liliokusanya nchi za Nigeria, Niger, Chad na Cameroun linaonekana halina faida kuwepo kwake katika maeneo hayo.